KUJIFUNGUA KWA OPERATION

KUJIFUNGUA KWA OPERATION


KARIBU sana ndugu msomaji wangu wa  Afya muhimu Blog. Leo nakuletea makala inayo husu kujifungua kwa operation.



Siku hizi hasa  kwa hapa taTanzan kumekuwa na wimbi kubwa  la wanawake wengi kujifungua kwa njia ya operation na imekuwa kawaida kabisa kuliko hata kwa njia ya  kawaida

Katika makala hii utapata  kujifunza  kuhusu

 - Sababu za kujifungua kwa operation

- Madhara ya kujifungua kwa operation

- Njia za kuepuka kujifungua kwa operation.

Sasa  soma hapa kwa  makini.



 SABABU ZA KUJIFUNGUA KWA OPERATION



Kuna sababu mbalimbali za kujifungua kwa operation ila  zifuatazo ni kuu katika sababu  hizo.



1. NJIA KUWA NDOGO.

Hii kwa  akina mama  wengi  huwapata   hasa  kwa  wale  wenye maumbo madogo   au  wanawake  wanene  ambapo  njia inakuwa ndogo kutokana na mafuta  mengi mwilini na kupelekea  kuubana  uke  na  kushindwa  kupitisha mtoto wakati wakutaka kujifungua.



2. UMRI.

Hii  ni  hasa  kwa  maeneo ya  vijijini  huwa inafanya  kuwaua mabinti wengi  wakati wa kujifungua. Inatokana na  kuolewa  wakiwa  na  umri mdogo  ambapo  njia ya  uke  huwa  inakuwa  ndogo  na  kushindwa  kupitisha mtoto wakati wa kujifungua.

Ndio maana  hii inapigwa  vita  Takriban ulimwengu mzima  kwa  kuepusha  ndoa za utotoni.



3. MTOTO TUMBONI.

HAPA kuna sababu kuu mbili.



i.) Mtoto kukaa  vibaya  tumboni.

Mtoto kukaa  vibaya  tumboni  ni  ile hali ambapo mtoto badala ya kutanguliza kichwa  basi  inatangulia  miguu. Hapa  ni  hakuna  jinsi itabidi operation ihusike.

Mbeleni  utapata  kujua  kwanini  Mtoto anakaaa  vibaya  Tumboni.



ii.) Mtoto kuwa mkubwa.

Mtoto kuwa  mkubwa  inatokana  na  chakula  ambacho  alikuwa  anakula  mama  wakati wa ujauzito wake hasa  chakuwa  chenye  winyi wa fat(mafuta). Hii inamfanya mtoto kuwa mkubwa na  kushindwa  kupita  katika njia ya uzazi.



4.) HORMONES

 . (mfumo wa kemikali-taarifa  za mwili)

Hormone inayohusika  katika  kujifungua mtoto  inaitwa OXYTOCIN hii  kwa  wengi  huita UCHUNGU . Hormone  hii   ikiharibiwa   au ikiwa  chini hupelekea  kuwepo kwa  uchungu mdogo au pengine kutowepo kwabisa na  kupelekea  operesheni.



5.) MTOTO KUFIA TUMBONI.

Mtoto kufia Tumboni  hapa  lazima operation  itumike  maana   taarifa ya kujifungua  huwa inatolewa  na  Mtoto mwenyewe  akiwa tumboni kuwa Tayari Amesha kuwa na  tayari kuanza maisha  ya  Dunia. Hivyo akiwa amefia TUMBONI hapo  hamna  namna  nyingine.



       MADHARA YA KUJIFUNGUA KWA

                          OPERATION



1.) KIFO (mama/mtoto)



Operation ikifanyika inaweza ikasababisha  kifo  aidha ni kwa mama au mtoto kama  itafanyika   vibaya.

Hivyo  operation siyo  jambo la  kuzoea  ni  jambo  la  hatari.



2.) UPUNGUFU WA DAMU.



Wakati wa operation  kunaweza  kusababisha kupungukiwa kwa damu nyingi  hii ni  kwa mama  anaye  jifungua  na  muda  mwingine   hupelekea mtu Akafariki  kutokana  na   upotevu mkubwa wa damu mwilini.



3.) MAAMBUKIZI YA MAGONJWA MENGINE.



KATIKA operation  kumekuwa  na  maambukizo mengi  sana  ya magongwa  hasa  VVU/UKIMWI.

Hii inaweza  kutokea  maambukizi  katika  vifaa  vya  kufanyia operation, au maambukizi  kutoka  kwa  Mama kwenda  kwa mtoto endapo  Damu ya mama na  ya  mtoto  zikigusana. Hivyo  huwa  inahitaji umakini  sana  kama mama atajifungua  kwa operation na  pia kama ni Mwathirika wa VVU au UKIMWI.





   JINSI YA KUEPUKA KUJIFUNGUA KWA

         NJIA YA OPERATION



YAFUATAYO ni  mambo mbalimbali ambayo umaweza  zingazi wakati wa ujauzito ili kuepukana na  Tatizo la  kujifungua  kwa  operation.



1.) LISHE.



HAPA tunaongelea  swala zima la  Ulaji wa Mlo kamili. Hii hufanya  kujengeka  vizuri kwa  mwili wa mama na mtoto  na hata pia  viungo  vya  uzazi kuwa imara  na   swala zima pia  la UCHUNGU wakati wa kujifungua  linakuwa  La  kawaida kwa sababu  mwili unakuwa  unazalisha  UCHUNGU mwingi  na  kufanya  kujifungua  kwa njia ya kawaida na  kwa haraka zaidi.



 NB; EPUKA kula vyakula  vyenye MAFUTA MENGI hasa  pindi ujauzito utakapo fikia  umri wa  miezi SITA .  Hii itapelekea kuuepusha  mwili  kuwa  mkubwa ili  isije  leta  swala la njia  kuwa ndogo   PIA  inasaidia  kutokunenepa kwa mtoto akiwa  tumboni  isije sababisha kushindwa  kupita  wakati wa kujifungua.



2.) EPUKA KUTUMIA MADAWA MBALIMBALI BILA YA USHAURI WA DAKTARI.



Wanawake  wengi wamekuwa wakijisababishia  kujikujif kwa operation  kwa  kisa cha  kutumia  madawa mbalimbali bila ya ushauri wa daktari.

Hasa  wamekuwa  wakitumia  Dawa za  kuondoa maumivu (Pain Killers)  na bila kutambua  viambata vyake  katika utengenezaji wake. Hupelekea kupungua kwa Uchungu kwa  sababu  mwili unakuwa  umehangaishwa na kemikali mbalimbali.



Pia kuna baadhi ya dawa  hupelekea  kutoka kwa mimba enyewe ( PLACENTAL DETACHMENT). Ndio Maana  huwa  Wanashauriwa  kwenda Clinic  wakati wa Ujauzito ili kujua Maendeleo ya Afya ya Mama na Mtoto.



3.) EPUKA KUTUMIA VINYWAJI VYA VIWANDANI.



Hapa sana sana tunaongelea  Soda na baadhi ya vinywaji vingine  ambavyo  hupelekea  kuongezeka kwa  sumu mwilini na  kufanya  maendeleo mabaya ya mtoto akiwa tumboni.

Vinywaji vingine  hufanya Mtoto kufariki akiwa Tumboni.

Unashauriwa ukiwa kama mama mjamzito  pendelea  matunda kwa wingi na  mbogamboga  ili kuupa mwili kinga  na kuondoa  sumu mwilini.



4.) EPUKA VITU VYENYE CAFFEINE NYINGI.



Hasa  hii hupatikana kwenye vinywaji kama Kahawa, Cocacola, Energy drink n.k

Hii kwa mama mjamzito hatakiwi kabisa kutumia  maana  kwake yeye anaeza ona ni sawa  lakini  madhara makubwa yanampata mtoto maana  hupelekea mzunguko mkubwa  wa  damu na mapigo ya moyo yakienda  kasi   hufanya  mtoto akafariki.



5.) EPUKA MATUMIZI YA VILEVI VYOVYOTE.



Vilevi kama sigara, pombe na madawa ya kulevya  hupelekea  kusababisha  kifo kwa mtoto au pia  kupungukiwa kwa  nguvu za  kujifungua   sababu ya  uchungu mdogo  ulio haribiwa  na matumizi ya  vilevi.





6.) MUONE DAKTARI MARA KWA MARA UKIWA MJAMZITO.



Kama ukizingatia haya  hutaweza  kujifungua kwa operation.

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

FAIDA YA KAROTI MWILINI