KITUNGUU SAUMU

KITUNGUU SAUMU

KITUNGUU SAUMU kimekuwa kiungo  kikubwa  sana  kwenye maisha  yetu ya kila siku kwa upande wa chakula kama pilau mboga za michuzi na vingine kadhalika.

Pia  wengine huvitumia kama  dawa  lakini  wengi wao  hutumia  wa  hisia  tu  bila kujua   kinatibu nini na  kinasaidia  nini moja kwa moja. Hii ni  kutokana na  asilimia kubwa  ya watu  hasa  kwa jamii ya  Africa  hudhani  kuwa  kila kitu chenye ukali au uchachu basi ni dawa, kiukweli  ni  vingi nina tiba  ila  hatujui ni  nini inatibu na  kama ikitumiwa  vipi.

- Karibu sasa uweze  kujua kuhusu faida, madhara na matumizi ya Kitunguu saumu mwilini.


  FAIDA ZA KITUNGUU SAUMU:

- Huondoa sumu mwilini.
Kutokana  na  kuwa na  kemikali  ambayo huitwa Alicin ambayo  husaidia kuondoa  sumu mwilini  (free radicals) zinazo kuwepo kwenye misuli, mishipa, damu na tushu mbalimbali za mwili.

- Kuongeza Kinga za mwili.
Kama ilivyo elezwa hapo mwanzo  kwa  kuwa na  uwezo wa kuondoa sumu  basi  huongeza kinga  za mwili.

- Ina uwezo wa kupunguza mafuta mwilini na kwenye mishipa ya damu ( cholesterol). Hivyo kwa watu wenye tatizo la uzito mkubwa wanashauriwa kutumia sana vitunguu saumu.

- Huongeza nguvu za kiume.
Hii ni  kutokana na  uwezo wa  kutanua mishipa ya damu hivyo pia mishipa ya damu ya uume hutanuka  na kuongeza  Umbo, urefu na nguvu za uume.

- Huondoa tatizo la maumivu ya kichwa.
- Huondoa mafua, maumivu ya kifua na kikohozi.
- Huondoa chunusi, madoadoa na mabaka baka  katika ngozi na usoni pia.
-Husaidia  mmeng'enyo wa chakula.
- Husaidia  kutibu majeraha na michubuko katika mwili kwa haraka.
- Kwa wanawake  huwasaidi  kupunguza maumivu ya tumbo  hasa  katika  siku zake.
- Hutibu tatizo la kutokwa kwa uchafu na harufu mbaya ukeni.
- Kinaleta ladha katika  chakula.
- Kuondoa usaa  kwa mwenye jipu .
- Kunafanya kazi ya Kuamsha kazi mbalimbali za mwili ( ku boost uzalishaji wa seli).

Hizi ni baadhi ya faida na umuhimu wake  katika mwili.

  JINSI YA KUTUMIA KITUNGUU SAUMU

1. KWA MATIBABU YA NDANI YA MWILI.

- Kwa matumizi yatakayo kuwa kama tiba ndani ya mwili kama kuondoa sumu, nguvu za kiume , ngozi n.k   Fanya hivi
→ Kila asubuhi menya punje sita hadi kumi meza kama unavyomeza dawa , unaweza  kuvimeza  jwa  kutumia maji au maziwa  kama  huwezi  kula  vikavu. Tumia  wakati  tumbo halina kitu  ili  kuvipa  uwezo wa  kuingia kwenye damu  kwa urahisi na  haraka.
Ukifanya  hivi ndani ya wiki tatu  lazima uone mabadiliko.

2. KWA KUONDOA CHUNUSI USONI.

- Menya punje kadhaa  kisha  vipondeponde   hadi kuwa  kama tope zito, baada ya hapo  paka  usoni na  uache  kwa muda wa dakika 15 hadi 20  ili  viweze  kupasua vipele na kupenya  kwenye ngozi.
Fanya  hivi  kabla  ya  kuoga au muda ambao upo  free.

3. KWA WANAWAKE KATIKA KUTIBU UKE.

- CHUKUA kipande/punje moja ya kutunguu saumu kisa  kifunge na uzi (hakikisha  uzi umekaza vizuri punje hiyo)
Kisha kiingize  ukeni huku  uzi ukiwa  upo nje  kwa ajili ya  kukivuta nje.
Fanya  hivi  wakati wa kulala  na  asubuhi  kitoe kwa  kuvuta uzi nje.
Fanya  hivi ndani ya wiki   na matokeo utayaona.

4. KWA WANAOPIKA.

 - Kupika Kitunguu saumu kinatakiwa  kuwekwa  mwishoni  na  kisiive  sana  ili kuepusha  kuua  Kemikali tiba (ALICIN).
Ni vizuri ukahakikisha  kila chakula chako kisikose kitunguu saumu  ili iwe kama tiba na kinga endelevu kwako

  MADHARA YA KITUNGUU SAUMU.

Madhara ya kitunguu saumu ni kama ifuatavyo;

- Harufu mdomoni.
Kama ukila  kitunguu saumu  kibichi  huacha harufu  mdomoni  na kwa wengine  huwaletea kichefuchefu.

- Kwa watoto wadogo  hawatakiwi  kuvitumia vikiwa vibichi maana  vina uwezo wa kutanua  mishipa ya damu na  muda mwingine  kusababisha kupasuka kwa  baadhi ya mishipa.

- Mzio.( Allergies)
Kuna watu wakila kitunguu saumu hupata mzio na  kuharisha au kuumwa tumbo.

- kwa wengine kinaweza  kuwaletea  kichefuchefu na  kuwapelekea kutapika.


==> Wamana wajawazito na watoto wadogo  hawaruhusiwi  kutumia  hasa  vikiwa  vibichi  na  kwa  wenye  matatizo ya  Mzio.

All the best in Your Health

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

KUJIFUNGUA KWA OPERATION

FAIDA YA KAROTI MWILINI