KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI

KUTOA HARUFU MBAYA MDOMONI.

Kutokwa na harufu mbaya mdomoni  ni moja ya tatizo  ambayo  baadhi ya watu katika jamii hupata  na  kuwafanya  upweke kutokana na  adha hiyo.

  SABABU YA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI.

Kuna sababu mbalimbali zinazo sababisha mtu kutokwa na harufu mbaya mdomoni Lakini sababu kuu ni  FANGASI.

1. Fangasi.
Faghasi  kwa kawaida  huwa  ikiwepo sehemu yoyote ya mwili  hufanya  sehemu hiyo kutoa harufu mbaya.
Basi fangasi hii ikikaa  katika mdomo kwenye Fizi, Meno au ulimi  hufanya   kutuka kwa harufu mbaya mdomoni ambayo  hata mtu akiswaki mara nyingi au kusukutua bado itakuwa  haisaidii kitu.

2. Kutosafisha kinywa mara kwa mara.
Kusafisha kinywa mara kwa mara  husaidia  kuondoa mabaki ya chakula  ambayo yakikaa kwa muda mrefu kwenye kinywa basi husababisha  kutokwa kwa harufu.

3. Kula vitu vinavyo weza kutoa harufu kali kinywani.
Ulaji wa vitu kama vitunguu maji au saumu hasa vikiwa vibichi, Kabichi mbichi, samaki  n.k husababisha  kinywa kutoa harufu.

  MADHARA YA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA KINYWANI.

Madhara ya kutokwa na harufu mbaya kinywani ni kama ifuatavyo:

- Kutengwa na watu.
Hii huathiri sana  saikolojia ya mtu binafsi na  kujikuta mpweke sana  kwa kuwa watu humwepuka kutokana na harufu kali  ambayo  anatoa kinywani.

- Kichefuchefu.
Harufu mbaya kinywani husababisha  muda mwingine mtu kujihisi kichefuchefu na mwingine  hadi kutapika  kutokana na harufu  kumkera.

- Kuharibu mahusiano hasa kwa wapenzi.
Harufu mbaya kinywani hupelekea kuvunja mahusiano ya kimapenzi kutokana  na  mmoja wapo kushindwa  kuwa na mwenzake  kutokana   na harufu kali anayo toa kinywani.

- Kutokujiamini.
Mtu mwenye tatizo hili huwa hawezi kujiamini hasa anapokuwa na watu na anapotaka   kuzungumza na mtu kwa kuhofia kusikika kwa  harufu  kali anayo toa kinywani.
Hii pia  huwafanya  hata  vijana wengi  walio na tatizo hili  kushindwa kujiingiza katika mahusiano ya kimapenza kwa  kuhofia  tatizo lake.


  NAMNA YA KUEPUKANA NA TATIZO HILI.

ILI uweze kuepukana na tatizo hili  basi  fanya  yafuatayo:

- Safisha kinywa mara kwa mara hasa  kwa  kutumia  chumvi  au ndimu  ambayo  inasaidia kusafisha  sehemu zote zenye michubuko ambazo  zinaweza  kupelekea  kukua kwa fangasi.

- Kila baada ya mlo wako wowote   sukutua kwa maji safi  ili kuzuia  mabaki ya chakula  kuganda kwenye meno au fizi.

- Safisha ulimi kwa maji na dawa ya meno. Watu wengi  huwa wanasahau kusafisha ulimi  lakini  pia  ndicho  chanzo  cha  harufu kinywani.

- Tumia dawa zinazo ondoa fangasi kinywani.

- Epuka ulaji wa vitu vinavyo acha harufu mbaya kinywani. Kama vutunguu   na kama utatumia  basi safisha kinywa  ili  usibaki na harufu hiyo.

#Kama tatizo litazidi basi  nenda kwenye kituo cha afya onana na mtaalamu wa kinywa na meno.





  All the best in your health

-

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

KUJIFUNGUA KWA OPERATION

FAIDA YA KAROTI MWILINI