OSTEOPOROSIS

*"MADA YA LEO : UGONJWA WA OSTEOPOROSIS"*

Osteoporosis ni nini  ? 🤷‍♂

Osteoporosis ni Ugonjwa Sugu wa Mwili Kujitafunia Virutubisho Vilivyo Kwenye Mifupa  na Kuvitumia Kwa Mahitaji Yake.

Hali  hii  husababisha Kupungua Kwa Umahiri wa Mifupa  ( Bone Density ) na Kuifanya  iwe hafifu na Kumegeka hovyo.

Ugonjwa huu ndiyo Maana Ukapatiwa Jina  la Umaarufu la *Silent Disease* Kwani Mara Nyingi  hujulikana Pale tu Mtu  anapoanguka au Kujigonga na Kuvunjika ( Kwa Urahisi Sana au Kupata Fructure  ) Tofauti na mtu  asiye na tatizo  hili.

• Osteoporosis ni hali  inayojitambulisha Kwa Kupungua Kwa Ujazo wa Mifupa , Kupungua Kwa Nguvu za Mifupa na Kufanya Kuwa Rahisi Kuvunjika .

• Osteoporosis huufanya Mfupa  Kuwa na Vijitundu Vingi Isivyo Kawaida Unaoweza  Kushindilika ( Kupungua Ukubwa Kwa Kugandamizwa ) Kama Sponji .

• Mfupa  wa Kawaida Hujengwa Kwa Protein , Collagen na Calcium ambayo huupa Mfupa  Ugumu.

• Osteoporosis husababisha Mifupa Kuwa Dhaifu na Inayovunjika Kirahisi Kiasi Kwamba Kuanguka Kidogo tu au Kujikunja ama au hata  Kukohoa Kunaweza Kusababisha Mvunjiko.

• Mvunjiko Unaweza Kuwa na Muundo wa Ufa  ( Kama Mvunjiko wa Nyonga ) Uti  wa Mgongo , Mbavu na Vifundo Vya Mikono ni Sehemu ambazo huathiriwa Zaidi na Osteoporosis Ingawa Mfupa  wa Sehemu Nyingine Yoyote Pia huweza Kuathiriwa.

• Mifupa ya Mwili Kwa Wakati Wowote huwa na Mabadiliko Ya Kujengeka , Kujiimarisha na Kujirekebisha  ( Bone Remodeling ) Kwa Kupitia Mzunguko Maalum wa Kusagika ( Osteoclast ) ambapo hutoa Madini yake ya Calcium Katika Mzunguko wa Damu.

• Osteoporosis ni Upungufu wa Umahiri wa Mifupa ( Low Bone Mass ) Hutokea Pale ambapo Usagaji wa Mifupa ( Osteclast ) Uko Juu  Zaidi ya Ujengekaji wa Mifupa ( Osteoblast ) .

• Binadamu hufika  Kilele Cha Ujenzi wa Mifupa Kati ya Umri wa Miaka 25 - 30 , Kwani Kabla ya Umri huu Mifupa hujijenga za Kusagika Kwa Kiwango Kidogo Kama inavyotakiwa .

• Baada ya Umri wa Miaka 30 Usagikaji wa Mifupa huuzidia Kwa Kina Kikubwa Kuliko Ujengekaji wa Mifupa .

• Hivyo hupelekea Upungufu wa Umahiri wa Mifupa Unaojulikana kama Decrease Bone Density .

• Hii inatuonyesha Jinsi gani Madini ya Calcium ni Muhimu Kwani Ulaji wa Chakula Kisichojumuisha Calcium na Vitamin D ( Vitamin D husaidia Unyonyaji wa Calcium Kutoka  Kwenye Chakula ) husababisha Mwili Kutumia Calcium inayohifadhika Kwenye Mifupa .

• Ili  Calcium iweze Kujitoa Katika Mifupa ( Hifadhi Yake ) na Kutumika  Mwilini ( Katika Mzunguko wa Damu ) inabidi Mifupa Ipitie hatua ya Kujisaga na Kutoa Kirutubisho hicho Kinachohitajika na hivyo Kutuacha na Mifupa Dhaifu.


Inaendelea ..................

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

KUJIFUNGUA KWA OPERATION

FAIDA YA KAROTI MWILINI