UGONJWA WA KISUKARI

UGONJWA WA KISUKARI.
   (DIABETES).

Ugonjwa wa kisukari  ni moja  kati ya magonjwa tishio sana  hasa kwa karne hizi ambapo  Ugonjwa huu haichagui rika  na  kila  mtu anaweza kuupata  kutokana  na  sababu  mbalimbali.

KISUKARI inaweza  kuwa  sukari imeshuka  au imepanda mwilini na hivyo  kusababisha  mwili  kutokuwa  na ufanisi mzuri wa kazi zake  za  kila  siku.

AINA  ZA  UGONJWA WA KISUKARI.

KUNA aina kuu mbili  za  ugonjwa wa kisukari   Ambazo ni Diabetes Mellitus na Diabetes Insipidus.

1. DIABETES MELLITUS.

HII ni kisukari kilicho zoeleka sana  na  asilimia  kubwa  ya  watu  hasa  watu wazima   hupata   huu   kutokana  na  Mfumo wa maisha.
– Aina hii ya  kisukari  imegawanyika katika makundi mawili.

i.) Diabetes Type 1.
Hii  ni  kisukari ambacho  mtu  hupata  kutokana na  kongosho  kushindwa kufanya kazi vizuri  kwa  kushindwa  kutoa  kemikali ambayo   hutumika  kufanya  msawazo wa  viwango vya sukari katika mwili. Hormone  hii  huitwa INSULIN  ambayo  hugeuza  Glucose kuwa Glycogen  na  kuhifadhiwa mwilini. Lakini  inapo  feli  kutolewa   basi  mtu  hukumbwa na Tatizo la  kujawa na sukari nyingi  mwilini.

ii.) Diabetes Type 2.

Hii  ni aina  ya  kisukari  ambapo  huwapata  sanasana  watoto na  vijana  wenye  umri mdogo.
Hii  ni  ile  Sukari ya  kurithi  ambapo  mtoto  huzaliwa  nao.
Hii ni  kutokana  na  kurithi kutoka  kwa  mzazi  au  vinasaba  kutoka  katika  ukoo wake.


2. DIABETES INSIPIDUS.

AINA hii ya  Kisukari  huwapata  hasa  watu  wanao tumia  Pombe kupita kiasi  na wanao tumia  sigara au madawa ya kulevya  kupita  kiasi  na hivyo  kufanya   figo kushindwa  kuchuja  damu  na  kuachilia  maji  mengi  kutoka  kwa  wingi mwilini hasa    kwa  njia  ya  mkojo.

→ Figo ni Ogani  Muhimu  sana  katija  swala  la  kuchuja  damu  na   kuisafisha  kwa kutoa  sukari zilizi zidi na  kuondoa   takataka  nyingine kwenye damu.
Kwa  watumiaji wa  madawa ya kulevya na Pombe  huwa  wanaathiri  Ubongo  Ambapo  Tezi kuu  Ya  PITUITARY  GLAND iliyopo katika ubongo hushindwa  kutoa  homoni Inayoitwa ADH (Anti-duretic hormome) au Vapopressin ambayo kazi yake  ni  kukabiliana na   Vitu vyovyote  vile vinavyo sababisha  Upotevu wa maji mwilini, hivyo  ikihitilafiwa na  Keimikali  hizo basi  hupelekea  Maji kutoka  kwa  wingi na  sukari  nyingi  kuwepo  mwilini.
- Wagonjwa wa  aina  hii ya  kisukari huwa  wanatoa mkojo  ulio  safi na mara nyingi  hupata  kiu  na  kusikia haja  kila mara.

  SABABU ZA KISUKARI.

KISUKARI  kinasababishwa  na  sababu  kuu Mbili. Nazo ni :-

1. MFUMO WA MAISHA.

MIFUMO ya maisha ya watu wengi  huwapelekea  kupata  ugonjwa  wa kisukari  kwa  matumizi  ya  vyakula  vilivyo na  asilimia kubwa ya kuleta  ugonjwa  wa  kisukari  mwilini.
Mfano kama:
- Matumizi ya sukari nyingi  kwenye vyakula.
- Matumizi ya  vyakula  vya  viwandani  ambavyo  vingi  huwekwa   sukari  nyingi  kama  Keki, biscuit, Soda  na  hata  baadhi  ya  peremende.
- Matumizi ya  pombe  na  vinywaji kama  soda na  Juices za  viwandani.

→ Pia  kuwa  na  uzito  mkubwa  husabaisha kupata  kwa  kisukari  kwa kuwa  mtu  huwa  na  uzito  ambao  hauendani  na  Umri na  kimo chake. Hivyo  watu  wenye OBESITY wamo hatarini kuupata  ugonjwa huu  kama hawatazingatia  mlo na mazoezi.

2. KURITHI.

KAMA ilivyo elezwa hapo awali  kuhusu  kisukari cha kurithi ambapo   ndicho kinacho fanya  marika yote  kuwa na uwezekano wa kupata  ugonjwa  huu ambapo mtoto  huzaliwa  nao  kwa  kurithi  katika ukoo wake. Hii ni  Maswala ya  vinasaba  vinavyo tembea  kutoka kizazi hadi kizazi  haina  tofauti  kama  mtu mwenye Albinism (Albino) anavyo pata  na  huu  ugonjwa  ndivyo  unavyo patikana.


  DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI.

- Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara.
  Hii ni kwa sababu mwili  hushindwa  kutunza maji.

- Kuhisi kiu mara kwa mara.
- Kuhisi njaa  mara kwa mara.
- Kupungua Uzito.
- Shinikizo la damu.
- Kupata  maambukizi ya magonjwa mengine ovyo ovyo.

   MADHARA YA KISUKARI.

Kisukari  kina madhara kadhaa  nayo ni:

- Kifo.
Kama mgonjwa hatochukua tahadhari mapema basi  anauweza kufariki  pindi  kadri itakavyo kuwa  ikzidi mwilini.

- Mishipa ya damu  Kubana.
Hii huitwa Artheroclerosis ambapo mishipa ya damu  hushindwa  kupanuka  na  kupelekea  presha  ya  damu  kuongezeka na moyo kwenda mbio  huku  ukijitahidi  kupitisha damu katika mishipa  hiyo.

- Macho kutokuona vizuri.
- Figo kushindwa kufanya kazi vuzuri na  pengine  kufeli kabisa.
- Ukosefu wa Nguvu za kiume na  kushindwa  kuzalisha  mbegu za kiume vizuri na  kupelekea  Ugumba.
- Kuwa na Vidonda visivyo pona.
- Kisukari pia husababisha Kiharusi (Stroke)


==> NDIO maana  huwa  tunashauriwa  kuangalia  afya zetu mara kwa mara  ili  kujua maendele ya miili yetu.


ILI KUEPUKANA A TATIZO LA KISUKARI...

- Badili mfumo wa maisha  kwa  kula  vyakula vilivyo na lishe kamili  na  kupunguza matumizi ya sukari kupita kiasi.

- Fanya japo mazoezi kwa nusu saa  kwa  siku. Ila kama  huwa unahisi uvivu  basi tembea  japo kwa  nusu saa  kwa  siku  ili  mwili uchangamke  na  kufanya  kuondoa mafuta na  sukari  zinazo baki mwilini kwa  kuzigeuza kuwa  nishati ya mwili.

- Epuka matumizi ya Pombe, Sigara na madawa ya kulevya  kupita kiasi.

-Epuka  matumizi ya  vinywaji vya viwandani  hasa  soda na  juices, vinywaji hivi huwa na sukari nyingi sana katika utengenezaji wake.

- Kula matunda  angalau aina tatu tofauti tofauti kila siku  na  mbogamboga.

- Epuka matumizi ya Mafuta mengi hasa  yale  yatokanayo   na wanyama.
- Tumia mafuta yatokanayo  na mimea kama alizeti na karanga.




All the best in Your Health

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

KUJIFUNGUA KWA OPERATION

FAIDA YA KAROTI MWILINI