UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

UPUNGUFU/UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME


Karibu sana ndugu msomaji wangu, Na leo tunaangalia  swala zima la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume.

- Katika dunia ya sasa  Upungufu wa Nguvu za Kiume  ndilo limekuwa tatizo kubwa  hasa kwa  vijana wengi  na kuhangaika huku na huko kutafuta suluhisho.
Hii huwafanya  vijana wengi  kuanguka  katika ndoa, mahusiano na hata  kiimani  kwa  kushindwa  kuwa na nguvu za kiume.

NGUVU ZA KIUME NI NINI...?

Nguvu za kiume ni  ile hali ya mwanaume kuwa na uwezo wa kisimamisha uume na  kuweza kuzalisha  na  hata  kujamiiana kwa ufasaha.

  SABABU ZA UPUNGUFU/UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

- Msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo unasababisha upungufu wa nguvu za kiume kutokana kupungu kwa  hisia za  kujamiiana  na  pengine  kumaliza   kabisa hizia  hizo  na  mtu  kujikuta  hana  nguvu za kiume.

- Kujichua/Punyeto.
Kujichua  hufanya kulegea kwa misuli ya uume kwa kuwa  mtu hutumia nguvu kubwa  katika kuubinya uume  na kuubana  mara kwa mara hivyo kusababisha uume  kulegea  na  kushindwa kusimama  vizuri.

- Matumizi ya Madawa ya kulevya na Pombe.
Matumizi ya madawa ya kulevya na pombe pia hupelekea  kupunguza nguvu za kiume kwa  kulegeza  mishipa ya damu na  kusababisha  damu  kutofika  vizuri katika uume.

- Matumizi ya Sigara.
Sigara ina sumu nyingi  ndani yake  kuu hasa  ikiwa ni  NICOTINE  ambazo  zikiingia  kwenye damu  hufanya mishipa ya damu  kuingiliwa na sumu  na  hivyo  kushindwa  kuwa na  nguvu kama awali na kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume.

- Matumizi ya dawa za kuongeza hamu ya kujamiiana na nguvu za kiume.
Dawa  hizi mtu akiwa anatumia mara kwa mara humfanya kuathirika kisaikolojia ambapo  anakuwa  hawezi  kujamiiana  bila ya kuwa na dawa hizo. Hatimaye kukosa  kuwa na nguvu za kiume.

- Matumizi ya madawa ya kuongeza umbo na urefu wa uume.
Madawa  haya  huwa na kemikali ambazo  huwa na lengo la kukuza  uume  lakini  mwishowe  dawa hizi  zikisha potea kwenye  misuli ya uume  hufanya  kutokuwa na  uwezo wa kusimama  kwa  kuweka  sumu katika mishipa na misuli ya uume.

- Ugonjwa wa kisukari.
Wagonjwa wa kisukari wapo sana  hatarini kwa  kupata  Ukosefu wa nguvu za kiume kwa mishipa ya damu kuingiliwa na sukari inayo fanya kudhoofika.

- SHOTI ya umeme.
Shoti ya umeme  huweza  kusababisha  mshtuko mkubwa sana  kwa mtu na  kumfanya   baadhi ya  hisia  kupotea  kwa  muda  hasa  hisia za mapenzi na  kurudi kwakwe  kusijulikane muda.
Ndio maana   unatakiwa kuwa mwangalifu na  umeme.

- Homoni za kiume kuzalishwa kwa uchache.
Homoni za kiume zikizalishwa kwa uchache  hupelekea mtu kukosa  hamu ya kujamiiana na hata  nguvu  kupotea na kuwa  muathirika wa  upungufu wa nguvu za kiume.

- USHOGA.
Mwanaume akisha kuwa shoga au mwenye SILKA za kike  hata  mfumo wake wa kisaikolojia  huathiriwa na tabia hiyo na  mtu kutokuwa na  uwezo wa  uume kusimama na  hata  hamu ya  kufanya mapenzi na jinsia  tofauti  hupotea na  kuwa  muhanga  wa   Tatizo hili.

- Malezi.
Mtoto  akiwa analelewa  katika jamii iliyo jawa sana na watoto wakike au kuishi na kukaa sana  na watoto wa kike  hufanya  kupoteza  hali ya uanaume na  hatimaye kuwa kama mtoto wa kike kabisa na  hata  kushindwa  kuwa na  nguvu za kiume  kabisa.

- Uzito mkubwa.
Uzito mkubwa hufanya  kupoteza  nguvu  za kiume kwa sababu  mishipa  kujawa na  mafuta hivyo kupelekea kushindwa kupitisha damu vizuri.


  JUNSI YA  KUEPUKA NA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME

- Epuka msongo wa mawazo.
 -Epuka  kujichua  mara kwa mara.
- Epuka matumizi ya sigara, pombe na madawa ya kulevya  kupita kiasi.
- Kama ni mzazi  ili  umuandae mwanao usimuweke  katika  makundi ya kike  kwa sana  maana itamuathiri  kisaikolojia.
-Fanya mazoezi ili  uepukane  na  Uzito.
- Pendelea  kunywa maji mengi  na  kula mlo kamili.
- Tumia vitunguu saumu na tangawizi mara kwa mara.

Pia  unashauriwa  kuto kusita kumuona mtaalamu wa Afya  hasa kwa maswala ya viungo vya uzazi vya mwanaume.



All the best in your health

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

KUJIFUNGUA KWA OPERATION

FAIDA YA KAROTI MWILINI