VIDONDA VYA TUMBO

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO (Peptic Ulcer Disease).
Vidonda vya tumbo ni uharibifu wa ukuta wa ndani wa tumbo (mucosa), uharibifu huo unaweza kupenyeza kutoka ndani mpaka nje ya ukuta wa tumbo.

Vidonda vya tumbo husababishwa na vitu vingi, lakini sababu kubwa zinazosababisha vidonda vya tumbo ni mbili (2):-
1) Maambukizi ya bakteria aitwae HELICOBACTER PYLORI (H.pylori), ambaye huambukizwa kwa njia ya mdomo kwa mdomo na njia ya choo.

2) Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za maumivu aina ya NSAID (nonsteroidal anti inflammatory drugs) mfano- ASPIRIN,PARACETAMOL,IBUPROFEN,DICLOFENAC n.k

Sababu zingine zinazopelekea kupata vidonda vya tumbo ni kama
-Unywaji wa pombe kupita kiasi
-Uvutaji wa sigara
-Kuwa na aina ya saratani tumboni inayosababisha acid kutolewa kwa wingi(gastrinoma)
-Kufanyiwa upasuaji mkubwa n.k

DALILI ZA UGONJWA...
 1) Maumivu makali ya juu ya kitovu (kiungulia),wakati mwingine maumivu huweza kukuamsha usiku.

2) Maumivu yanayotembea kutoka tumboni kuelekea mgongoni (pain radiate to the back).

3) Maumivu ya tumbo yanayopungua baada ya kula au yanayotokea masaa 2 mpaka 3 baada ya kula.

4) Kuhisi kichefu chefu na kutapika.

5) Tumbo kujaa gesi.

6) Kupungua uzito na kupoteza hamu ya chakula(appetite loss).

 7) Kupata choo cheusi (melena) au kutapika damu(hematemensis).

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO.
Vidonda vya tumbo vinatibika na kupona kabisaa, na si kweli kuwa vidonda vya tumbo haviwezi kutibika kama baadhi ya watu wanavyoamini.
#AfyaYakoniKipaumbele #AfyaZone #Afya

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA wa Pingili

KUJIFUNGUA KWA OPERATION

FAIDA YA KAROTI MWILINI